Friday, December 28, 2012

Saturday, December 29, 2012 TASWA Yawafunga Bagamoyo.

Kikosi cha timu ya Chama Cha waandishi wa habari za Mizhezo TASWA FC kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa kirafiki kati yake na timu ya Bagamoyo Veteran uliofanyika kwenye uwanja wa Mawanakerenge Mjini Bagamoyo jioni ya leo, ambapo timu ya TASWA FC imechapwa magoli 4-0 na maveterani hao kutoka mjini Bagamoyo,
Timu ya Waandishi wa habari ya TASWA FC imeshiriki katika mchezo huo ikiwa ni moja ya programu ya mkutano wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika kesho kwenye hoteli ya Kiromo View mjini Bagamoyo ambapo utafunguliwa na Ridhiwani Kikwete na Kufungwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ndugu Assah Mwambene.

Hiki ndiyo kikosi cha timu ya Bagamoyo Veteran kilichotoa kichapo kwa timu ya TASWA FC mjini Bagamoyo leo.

Baadhi ya waandishi wa habari ambao ni mashabiki wa timu hiyo wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo.

No comments:

Post a Comment