KLABU ya Real Madrid imejiweka kwenye
nafasi nzuri ya kwenda Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya
usiku wa jana kuilaza Galatasaray mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Bernabeu.
Cristiano Ronaldo alifunga bao la kwanza
mapema kipindi cha kwanza dakika ya tisa kabla ya Karim Benzema kufunga
la pili dakika ya 29.
Gonzalo Higuain aliyetokea benchi
kipindi cha pili alifunga la tatu kwa kichwa dakika ya 73 na kuwafanya
Madrid waende kwenye Uwanja wa Turk Telecom Arena Jumanne ijayo kifua
mbele.
Didier Drogba aliyeiongoza Chelsea
kutwaa taji hilo la Ulaya msimu uliopita, jana alipatya nafasi mbili
nzuri lakini akashindwa kuzitumia.
Katika mchezo huo, kikosi cha Real
Madrid kilikuwa: Diego Lopez, Varane, Ramos, Coentrao, Khedira, Ronaldo,
Ozil/Modric dk80, Alonso, Essien, Di Maria/Pepe dk86 na Benzema/Higuain
dk65.
Galatasaray:
Muslera, Dany Nounkeu, Kaya, Eboue, Altintop/Bulut dk78, Inan, Felipe
Melo, Riera/Amrabat dk83, Sneijder/Zan dk46, Yilmaz na Drogba.
Katika mchezo mwingine jana, Malaga na Borussia Dortmund zilitoka sare ya bila kufungana.
Kitu na boksi: Cristiano Ronaldo akifunga bao la kwanza dhidi ya Galatasaray Uwanja wa Santiago Bernabeu
Karim Benzema akishangilia bao lake
Malalamiko: Didier Drogba akilalamika
La tatu kiulainiii: Gonzalo Higuain alifunga bao la tatu kwa kichwa
Mpambano wa wanaume: Sergio Ramos
(kushoto) akipambana na Didier Drogba kipindi cha pili jana ambaye
alianguka kama anavyoonekana picha ya chini
Mpiganaji: Ronaldo akipambana dhidi ya wachezaji wa Galatasaray
No comments:
Post a Comment