Tuesday, April 23, 2013

BALOZI SEIF NA WIKI YA USALAMA BARABARANI ZANZIBAR.

1
        Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi

Na Miza Othman – Maelezo Zanzibar                                  

Imeelezwa kuwa ikiwa kutakuwa na  ushirikiano na uadilifu baina ya watoaji  leseni za Udereva na  Jeshi la Polisi nchini itapelekea kupunguza  ajali
za Baraabarani zisizokuwa za lazima.
  1. yameelezwa na  Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  wakati alipokuwa akizungumza na Wananchi, Wanafunzi  pamoja na Madereva wa vyombo vya moto kwenye  uzinduzi wa wiki ya usalama barabani katika ukumbi wa Salama, Hoteli ya  Bwawani Mjini Zanzibar .
  2. Seif  amesisitiza Umakini katika  utoaji wa leseni na kuwataka Madereva  kufuata Sheria wakati  wanapoendesha vyombo ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika kwa wananchi wanaotembea kwa  miguu na wale wanaoendesha vyombo vidogo vidogo.
“Katika kuyafikia malengo ya mpango wa miaka kumi ya usalama barabarani natoa wito kwa madereva kutoendesha mwendo wa kasi wanapokuwa barabarani, kutii sheria, kuwajali watumiaji wengine wa barabara ikiwa ni pamoja na waenda kwa miguu, wapanda baskeli na watu wenye mahitaji maalum” Alisema Makamu wa pili wa Rais.

Ameahidi kuwa Serikali kwa upande wake  itahakikisha kuwa inasimamia kwa ukamilifu  sheria za barabarani na kuwachukulia hatua wale wote wanao kaidi kufuata sheria hizo.

Ameongeza kuwa Serikali itahakikisha kuwa barabara zinazojengwa zinakidhi viwango ikwa ni pamoja na uimara wa barabara zenyewe , upana pamoja na kuwekwa alama zote muhimu zinazohusu usalama wa  barabarani.

Nae Kamishna  wa Jeshi la Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa amesema  ni vyema kamati  ya  mawasiliano kulishirikisha  Jeshi la Polisi  wakati wanapotoa maamuzi  katika masuala ya ujenzi wa barabara ili na wao waweze kutoa mchango wao kabla ya ujenzi kuanza.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya  Dokta Ahmed Jidawi  ameshauri madereva kufanyiwa uchunguzi  wa kiafya  kabla ya kupatiwa leseni  kama vile kuchunguzwa akili na hata macho jambo ambalo litapelekea  kupata madereva  walio bora .

Mkurugenzi wa Miundo mbinu na Mawasiliano amekemea tabia mbaya inayofanywa na baadhi ya watu  kuondoa alama za barabarani na kusema kwamba serikali itawachukulia hatua watakaobainika kufanya vitendo hivyo.

 Aidha amewanasihi madereva kuwa makini na kupunguza matumizi ya simu  wakati wanapoendesha gari kwani ni miongoni mwa vichocheo vya kutokea ajili za barabarani.
 Kauli mbiu ya wiki ya usalama barabarani mwaka huu  ni ‘’KUONDOA AJALI ZA BARABARANI NI  JUKUMU LETU SOTE’’.  


CHANZO/MjengwaBlogs.

No comments:

Post a Comment