MSHAMBULIAJI Wayne Rooney wazi
alionekana mwenye kupambana na tetesi za kuondoka kwake Manchester
United wakati wa mazoezi ya timu hiyo leo.
Huku timu hiyo ikijiandaa na mchezo wake
wa Jumatatu na Aston Villa, mshambuliaji huyo England alionekana
kujituma kwa vitendo licha ya tetesi za kuwa mbioni kuhamia PSG ya
Ufaransa.
Kocha wa United, Sir Alex Ferguson
alikuza tetesi za Rooney kuondoka baada ya kusema mshambuliaji huyo hana
tena uhakika wa namba katika kikosi cha kwanza.
Jino kwa jino: Wayne Rooney akiteleza kuchukua mpira miguuni mwa Ryan Giggs katika mazoezi ya Manchester United leo
Tabasamu mwanana: Rooney alikuwa katika ari nzuri leo licha ya tetesi za kuondoka Old Trafford mwishoni mwa msimu
Nje kwenye baridi? Sir Alex Ferguson akimuangalia Rooney na wachezaji wenzake wa United mazoezini leo
Kwa kuanza kwenye nafasi ya kiungo
mshambuliaji katika mechi mbili zilizopita, Rooney si mshambuliaji
chaguo la kwanza tena, na alitolewa baada ya kucheza ovyo katika mechi
iliyopita dhidi ya West Ham.
Ferguson alisema: "Tunachukua timu ya
ushindi na tulifanya hivyo kwa Stoke. Nitaendelea kufanya hivyo hivyo
(dhidi ya Aston Villa) Jumatatu.
"Kama ilivyokuwa Jumatano kumtoa ilikuwa rahisi, hakucheza vizuri kama Shinji Kagawa na tulipata bao tulilohitaji.
"Kuna mechi nyingi ambazo Wayne Rooney
amekuwa mchezaji bora zaidi ya wachezaji wengine, lakini katika usiku
huo, Shinji alicheza vizuri sana,".
Pointi tatu katika mechi ya Jumatatu pia
zitaifanya United ijihakikishie ubingwa wa Ligi Kuu ya England kwa mara
ya 20, iwapo jirani zao City watafungwa na Tottenham Jumapili.
Kupambana kuwa fiti: Wachezaji wa United, Anderson (kushoto) na Danny Welbeck, wakijifua kujiandaa na mechi dhidi ya Aston Villa
Mbadala? Ferguson amesema Shinji Kagawa alicheza vizuri zaidi ya Rooney Jumatano
No comments:
Post a Comment