Godbless Lema, Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Kupitia CHADEMA.
Jeshi la polisi mkoani hapa limemtia
mbaroni mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godless lema kwa tuhuma za
uchochezi kwa wanafunzi kwenye chuo cha uhasibu mwanzoni mwa wiki
katika vurugu zilizotokea chuoni hapo baada ya mwenzao kuuwawa juzi
usiku huko maeneo ya njiro jijini hapa.
Akizungumza na vyombo vya habari leo
ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani hapa kamishna msaidizi wa polisi
Liberatus Sabas alisema kuwa mh.lema alikamatwa huko nyumbani kwake
Njiro majira ya saa 9 usiku.
Sabas alisema jeshi hilo linaendelea
na mahojiano na mtuhumiwa na kuwa katika tukio hilo zaidi ya watuhumiwa
14 walifikishwa mahakamani jana na kuwa hao hawezi kuwaongelea kwani
kesi yao ipo kwenye chombo hicho cha sheria.
Pia kamanda sabas alisema kuwa mh.lema
anashikiliwa kutokana na vurugu zilizotokea juzi kwenye chuo cha
uhasibu na kuwa atafikishwa mahakamani siku ya jumatatu.
Kwa upande mwengine akijibu baadhi ya
maswali ya wanahabari kamanda alisema kuwazaidi ya hao 14 na Lema
hakuna mtuhumiwa mwingine aliyakamatwa kwani ilisemakana wakili wake
Albert Msando nae amekamatwa.
Mnamo siku ya jumatatu mwanafunzi
mmoja aliuwawa kwenye mitaa ya njiro hali iliyoleta tafrani hadi
wanafunzi hao walipoleta vurugu chuo hapa na polisi kutumia mabomo ya
machozi kuwatawanya sekeseke hilo lilimalizwa na jeshi la polisi baada
ya wanafunzi kutotii amri ya mkuu wa mkoa huo Magessa Mulongo na kuanza
kuingia barabarani kuandamana. Chanzo: www.fullshangweblog.com
CHANZO/MjengwaBlogs.
No comments:
Post a Comment