Marehemu Debora Riziki miaka 3 enzi za uhai wake
Riziki Mwangoka kulia anaetuhumiwa kumzika mtoto wake akiwa hai
Hapa maiti ya mtoto Debora ikiwa imetolewa nnje mara baada ya kufukuliwa ndani ya nyumba ya baba yake mzazi
TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI TUNAZOZIONYESHA
Mwili wa marehemu Debora ukionyeshwa kwa mzazi na kudhibitisha kuwa ndiye mwenyewe aliyemfukia
Mwili wa mtoto Debora ukiandaliwa kwa kuzikwa kwa heshima zote
Mwili wa Debora tayari kwa kuzikwa
Hatimae sasa Debora anazikwa
Mara tu baada ya mazishi baba mzazi wa Debora anapelewa kituo cha polisi Tukuyu
Mama mzazi wa marehemu Debora asimulia kisa chote
Mama mzazi wa Marehemu, Esther Mwambenja, alisema kabla ya tukio hilo kutokea kulikuwa na viashiria vingi vya mumewe kufanya ukatili
Bibi wa marehemu Debora
Tukiwa na baadhi ya waandishi wenzangu tukiendelea kupata historia fupi ya marehemu Debora toka kwa mama yake mzazi
Novemba 15 mwaka 2012 serikali ya kijiji chini ya Mwenyekiti, Lutengano Mwakyoma na mashahidi watano wakiwemo wazazi na ndugu zake, walinikabidhi barua ya kuridhia kuondoka na mwanangu, huku ikimuonya mume wangu kutorudia kosa hili la kumuiba mtoto hadi hapo atakafikisha miaka saba.
Dada
wa marehemu Debora, Neema Stevini(5) kulia ambaye ni mtoto wa kufikia
wa baba mzazi wa marehemu, akisimulia jinsi mdogo wake alivyoibwa ,
alisema kuwa anakumbuka mara ya mwisho ilikuwa jioni majira ya saa 12
jioni.
“Nilitaka
kwenda nao, lakini baba Debora akaniambia nirudi kuchochea moto ndani
na niliporudi nikakuta wameondoka na nilipokimbilia sana siku waona”
alisema kwa masikitiko Neema.
MKASA
wa baba kumuua mwanae kwa kumzika akiwa hai kutokana na mgogoro wa
ndoa, umezidi kuibua mapya, baada ya mama mzazi wa marehemu ,Debora
Riziki (3), kusimulia mkasa mzima .
Akizungumza
kwa hisia kali, katika mahojiano maalumu na Mbeya yetu kijijini kwake
Ibula, katika kata ya Kiwira, wilayani Rungwe, Mama mzazi wa Marehemu,
Esther Mwambenja, alisema kabla ya tukio hilo kutokea kulikuwa na
viashiria vingi vya mumewe kufanya ukatili.
Alisema
tukio la mzazi mwenza huyo kumwiba mtoto na kwenda kumfanyia ukatili
huo wa kinyama lilikuwa la pili, baada ya awali kumuiba akiwa na miaka
miwili na miezi mine na alimrudisha kwa maandishi ya serikali ya kijiji.
Alisema
katika tukio la kwanza la mtalaka wake huyo kumuiba mtoto wao huyo,
lilitokea Septemba mwaka 2012, baada ya wiki chache za kumfukuza katika
nyumba waliyokuwa wakiishi katika kitongoji cha Iponjola, kijiji cha
Asenga, nyumba iliyotumika kuzikwa mtoto huyo.
Alitaja
sababu za yeye kufukuzwa ni ugomvi uliotokana na yeye kuhoji sababu za
kuficha fedha kiasi cha sh. 120,000 zilizotokana na wao kwa pamoja
kufanya kazi ya kibarua katika mashamba kijijini hapo na baada ya
malipo kutolewa mtalaka wake huyo alionesha kiasi kidogo cha sh.80,000.
Alisema
ugomvi huo ndio ulisababisha yeye arudishwe kwa wazazi wake, lakini
baada ya muda mfupi mwanaume huyo alimfuata na kumbembeleza ili
warudiane na alipogoma aling’ang’ania aondoke na mtoto .
“Nakumbuka
ilikuwa Novemba mwaka jana baada ya mimi kuondoka nyumbani kwake na
kurudi kuishi hapa nyumbani, siku hiyo tukiwa shambani huyo bwana
alikuja hapa nyumbani na kumkuta mwanangu wa kwanza (Neema Steven )
niliyezaa na mwanaume mwingine” alisema Mwambenja.
Alisema
baada ya kufika eneo hilo majira ya saa mbili asubuhi alitumia ujanja
na kufanikiwa kumuiba mtoto na kisha kutokomea naye kijijini kwao
Asenga, hali ambayo ilisababisha kutoa taarifa kituo cha polisi Kiwira.
“Unajua
kuwa baada ya kwenda kutoa taarifa polisi walitusaidia kufika kijijini
kwao ambapo serikali ya kijiji ilikubali nimchukue mwanangu kwa
kuwekeana mkataba wa kisheria kwa mujibu wa sheria, kwani alikuwa chini
ya miaka saba”.
Aliongeza
kuwa Novemba 15 mwaka 2012 serikali ya kijiji chini ya Mwenyekiti,
Lutengano Mwakyoma na mashahidi watano wakiwemo wazazi na ndugu zake,
walinikabidhi barua ya kuridhia kuondoka na mwanangu, huku ikimuonya
mume wangu kutorudia kosa hili la kumuiba mtoto hadi hapo atakafikisha
miaka saba.
Tukio la pili la kuiba mtoto.
Alisema
tukio hilo lilitokea Novemba 29 mwaka jana 2012, ambapo alifika
nyumbani kwao majira ya saa 12 :00 na kumkuta dada wa marehemu kumchukua
mtoto akimdanga kuwa anaenda kusenya kuni eneo la jirani.
Aliongeza
kuwa baada ya kuona dada wa marehemu anang’ang’ania kwenda wote
alimuamuru arudi nyumbani kuchochea moto kwa kuwa kulikuwa kumeinjikwa
mboga na kukubali kurudi.
“kwa
mujibu wa maelezo ya mwanangu huyu wa kwanza alisema baada kurudi toka
ndani, alikuta baba yake huyo ameondoka na mtoto na tuliporudi na
kupokea taarifa hizo tulichanganyikiwa na kuanza kuhangaika hovyo”
alisema mama wa marehemu.
Mwambenja
alisema kuwa baada ya kucha siku ya pili asubuhi yake walienda kutoa
taarifa kituo cha polisi cha Kiwira ili waweze kupata msaada wa
kumtafuta, huku wakionesha barua ya makubaliano ya awali ya yeye kuwa na
haki ya kisheria ya kusimamia malezi ya mwanao hadi afikishe miaka
saba.
Alisema
baada ya kutoa taarifa hizo kituoni hapo, askari aliyekuwa zamu siku
hiyo alimtaka kutoa kiasi cha shilingi 50,000 ili fedha hizo wapewe
askari mgambo wa kwenda kijijini kwa mzazi mwenzake huyo, kwani tayari
walikuwa na taarifa kuwa alikuwa amekimbilia huko.
“Kutokana
na hali ngumu ya maisha tulikosa kiasi hicho cha fedha hivyo suala
hilo kubaki bila msaada wa polisi na pia hatukuweza kwenda kwa kijijini
kwao”.
Aliongeza
“sababu ya mimi kuwa mzito kuendelea kumfuatilia kijijini kwao kwa mara
ya pili ili kujua kama yupo huko na mtoto ilitokana na hofu
niliyoijenga, kwani awali tukiwa kwenye ugomvi alitamka maneno ya
vitisho kuwa endapo nitaendelea kung’ang’ania kumchukua mtoto pale
anapomchukua atakuja kumuua ili tukose wote”.
Hata
hivyo mama huyo mzazi wa Debora, alisema kuwa baada ya kuona hali hiyo,
aliendelea kuwasiliana na wifi yake , Bupe Mwangoka,ambaye ni dada
mkubwa wa mume wake anayeishi eneo la Isanga Jijini mbeya, ambaye
ndiye alisaidia kwa kiasi kikubwa kubainika kwa unyama aliofanya.
Maisha kabla ya tukio.
Akielezea
maisha yao kabla ya kutengana na baadae kuamua kufanya ukatili huo,
alisema aliwahi kumtamkia maneno makali wakati akiwa na ujauzito wa
miezi nane .
Alisema
baada ya kuibuka ugomvi katika kipindi hicho, mwanaume huyo alimtaka
kwenda kuiuza mimba ile kwa mwanaume mwingine yeyote atakayempenda ili
asije akazaa mtoto ambaye atachanganya damu ya koo hizo mbili.
“Maneno
yale katika kipindi hicho sikuyatilia maanani kwani nilifikiri zilikuwa
ni hasira, lakini leo hii ndio najua maana ya ile kauli ” alisisitiza
Mwambenja.
Hata
hivyo alisema inashangaza kwani kuna wakati tukiwa katika maisha ya
kawaida kabla ya yeye kufanya tukio hilo, mara kadhaa alijutia na kuonya
juu ya matukio machafu yaliyojitokeza na kusikika ya watu kuuawa au
kuondolewa baadhi ya viungo vya miili yao.
Aidha,
alieleza mkasa mwingine wa mume wake huyo ni ule wa wao kufukuzwa
katika mji wa Kiwira walikokuwa wakiishi awali kwa kufanya shughuli za
umachinga.
Alisema
walitimuliwa na serikali ya mtaa katika mji huo kutokana na mumewe huyo
kutuhumiwa kuiba simu ya mkononi ambapo alipokea kipigo kikali na
baadae kufukuzwa.
Kutokana
na hali hiyo, mama wa marehemu Debora alisema yote yaliyotokea
amemwachia mungu na kwamba kama ingekuwa uwezo wake angeamuru naye
anyongwe, hivyo mamlaka husika zitajua cha kufanya.
Kwa
upande wake dada wa marehemu Debora, Neema Stevini(5) ambaye ni mtoto
wa kufikia wa baba mzazi wa marehemu, akisimulia jinsi mdogo wake
alivyoibwa , alisema kuwa anakumbaka mara ya mwisho ilikuwa jioni majira
ya saa 12 jioni.
“Nilitaka
kwenda nao, lakini baba Debora akaniambia nirudi kuchochea moto ndani
na niliporudi nikakuta wameondoka na nilipokimbilia sana siku waona”
alisema kwa masikitiko Neema.
Hata
hivyo uchunguzi wa Mbeya yetu umebaini kuwa marehemu Debora alifariki
dunia siku hiyo ya Novemba 29 mwaka jana, majira ya saa nne usiku baada
ya baba yake kufanikiwa kumuiba kutoka nyumbani kwa mama yake.
Inadaiwa
kuwa baada ya kufanikiwa kumtorosha baba huyo wa marehemu alitembea kwa
mguu umbali wa kilomita 50 kutoka kijiji cha Ibula alikomuiba hadi
nyumbani kwake kijiji cha Isange katika kata ya Isange.
Imeelezwa
kuwa baada ya kufika nyumbani kwake, baba huyo mzazi wa marehemu
alichimba shimo katikati ya sebule na kumchukua mtoto wake huyo akiwa
usingizini na kisha kumfukia akiwa hai.
“Mwanaume
Yule alikuwa katili sana, kwani baada ya kumfukia alichukua meza ya
chakula na kuiweka juu yake huku akiipamba kwa magazeti jambo ambalo
lilifanya ndugu zake wasigundue kirahisi” alisema mpasha habari.
Chanzo
hicho kilisema baada ya kufanya hivyo aliishi kwa wiki moja na baadae
kukimbilia Jijini Mbeya ili watu wasibaini juu kitendo alichofanya na
kwamba kila alipohojiwa na ndugu zake alisema mwanae huyo alimuweka kwa
rafiki yake Jijini Mbeya.
Hata
hivyo baada ya danadana za muda mrefu ndipo dada wa mtuhumiwa huyo
aliamua kutoa taarifa jeshi la polisi na kufanikiwa kumkamata akiwa
katika harakati za kutorokea wilayani Chunya na alipobanwa alifichua
siri ya alipo mwanae kwa kueleza kuwa alimuua na kumfukia ndani kwake.
Joseph Mwaisango
Ezekiel Kamanga
na
Venance Matinya.
No comments:
Post a Comment