*CAUTION/ILANI: Taarifa hii ni ya
awali kutoka kwa watu mbalimbali. Unafahamishwa tu kuwa na ufahamu wa
kinachoendelea. Taarifa kamili na iliyo rasmi itatolewa na vyombo
husika.
---
---
Taarifa katika mitandao jamii
zinaeleza kwamba usiku wa kuamkia leo, kijana mmoja wa kiume ambaye ni
mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (Arusha Institute of Accountancy)
aliyekuwa anasomea shahada ya kwanza Uchumi na Fedha (Bachelors Degree
in Economic and Finance) mwaka wa pili (BEF2), amefariki dunia baada ya
kuchomwa kisu.
SOMA ZAIDI
Taarifa za awali kutoka chuoni hapo
ambazo bado hazijathibitishwa na Jeshi la Polisi zinaeleza kwamba kijana
huyo anahisiwa kuchomwa kisu na vibaka wakati akirejea kwenye maeneo
yao ya malazi (hosteli) eneo la ESAMI.
Inaelezwa kuwa, kabla ya kufika
hostel, alipigiwa simu na mwenziye kuwa amsubiri ili waongozane pamoja
kuelekea hostel. Wakati akisubiri rafiki yake amfikie, ndipo watu
wasiofahamika waliokuwa wanadai wapatiwe fedha, walimvamia na kumchoma
kisu tumboni na shingoni.
Rafiki wa marehemu naye pia alichomwa kisu tumboni.
Mbunge wa Arusha Mjini, Mhe. Godbless
Lema alifika chuoni hapo na kuzungumza na wanafunzi hao ili kuwatuliza
baada ya kutaarifiwa kuwa kuna vurugu zilizotokana na hasira ya Wanachuo
kumshutumu Mkuu wa Chuo kutokuwapa msaada wa haraka hasa baada ya wao
kulalamika kwa muda mrefu sasa kuhusu hali duni ya usalama katika chuo
hicho.
Mwaka jana mwanafunzi mmoja aliuawa na katika nyakati tofauti,
wanafunzi wamekuwa wakivamiwa na kuibiwa vifaa vyao.
Taarifa pia zilimfikia Mkuu wa Mkoa,
Magessa Mulongo ambaye aliwasili chuoni hapo na kuzungumza na wanachuo
lakini ilizuka tafrani ndipo Wanachuo walianza kurusha mawe.
Kikosi maalumu cha Askari Polisi wa kutuliza ghasia, FFU, kipo katika eneo hilo kwa ajili ya kufanya kazi yake.
CHANZO:WAVUTI
CHANZO/Mjengwa Blogs.
No comments:
Post a Comment