Mhe.Abdallah Ulega kaimu mkuu wa mkoa wa lindi akikata utepe kuashiria uzinduzi wa huduma za matibabu ya madaktari bingwa sambamba na kupokea dawa na vifaa tiba kutoa NHIF ili kufanikisha zoezi ilo wanaoshuudia kulia ni mkuu wa wilaya ya lindi Mhe. Dr Hamid Nassoro,kaimu RAS Lindi Ndg John Likango na kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Taifa wa bima ya Afya bwn.Emanuel Humba
Wanachama na wananchi waliojitokeza wakimsikiliza mgeni rasmi hayupo pichani kwenye viwanja vya Hospitali ya Mkoa
Wanachama na wananchi mkoani Lindi
wametakiwa kujitokeza kwa wingi ili kutumia vyema fursa za huduma za
madakatri bingwa zinazoratibiwa na mfuko wa taifa wa bima ya afya katika
hospitali ya mkoa sokoine.
Hayo yalisemwa na mgeni rasmi kaimu
mkuu wa mkoa wa Lindi ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Kilwa mhe:
Abdallah Ulega wakati wa uzinduzi wa mpango maalum wa utoaji huduma za
matibabu kwa madaktari bingwa kutoka hospitali ya taifa muhimbili kwa
magonjwa ya akinamama, wataalam wa upasuaji na magonjwa ya moyo,figo na
shinikizo la damu uliofanyika katika viwanja vya hospitali ya sokoine
mjini lindi
Ni fursa adhimu ambayo wengi wetu hapa
mkoani Lindi,hatukuwahi kukutana nayo na sababu kubwa inawezekana ni
uwezo wa kugharamia safari ya kwenda huko wanakopatikana madaktari
bingwa sanjari na mlolongo mrefu wa taratibu za kitabibu ili
kuwafikia,lakini wenzetu,yani bodi ya wakurugenzi, menejimenti ya Mfuko
wa taifa ya bima ya afya wameiona changamoto hii na niseme wazi kuwa
mpango huu utakuwa unaokoa maisha ya watu wengi ambao hawakuwahi wala
kuwa na ndoto za kukutana na madaktari bingwa katika maisha yao.Ulega
alisema
Huduma hizi zimepangwa kufanyika kwa
siku saba hapa hospitalini kwetu Sokoine mkoani Lindi, hivyo nawaomba
madaktari wetu tutakaoshirikiana na hawa madaktari bingwa tujifunze kwa
maana ya kujiongezea ujuzi wa kitabibu ili watakapoondoka huduma hizi
zisitetereke bali ziboreke zaidi,hivyo wanachama na wanachi wa mkoa wa
Lindi na Mtwara wafike hapa kupata matibabu bora na stahiki.alisisitiza
mhe ulega
Pia aliwataka wananchi kujiunga na
mfuko wa afya ya jamii(CHF) ili waweze kunufaika kwa kupata matibabu mhe
ulega alisema...Maradhi hayabishi hodi wananchi hivyo kwa kuchangia CHF
uhakika wa matibabu ni mkubwa na pia utachochea maboresho ya huduma za
matibabu kwenye vituo vya afya,zahanati hadi hospitali mkoa wetu.....
Naye mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa taifa
wa bima ya afya ndg Emanuel Humba alisema mpango huu maalum wa kupeleka
huduma za madaktari bingwa kwenye mikoa ya pemebezoni , umezingatia
mahitaji ya msingi na ya wakati kwani ni dhairi wapo wanachama wetu
wengi waliopo vijijini,wana mahitaji makubwa ya huduma za madaktari
bingwa pasipo kuzipata kwa wakati.
Tunatarajia pia kufanikiwa kwa mpango
huu kutapunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali kubwa, hivyo
kutoa fursa kwa madaktari hao kutoa huduma kwa uhakika zaidi sanjari na
kuibua ukubwa wa mahitaji ya huduma za madaktari bingwa hapa mkoani
lindi na nchi kwa ujumla.
Alisema Mfuko umewagharimia madaktari
hao pamoja na utoaji wa dawa na vifaa tiba ,ili kufanikisha mpango huo
wenye thamani zaidi ya millioni hamsini,na mpango huu maalum utekelezaji
wake umeanzia mkoani Lindi na utakuwa ukitekelezwa kila baada ya miezi
mitatu na wanachama wa Mfuko watapata matibabu kwa kutumia kadi zao
sambamba na wananchi watapata huduma kwa kupitia utaratibu wa kawaida
ambao utakuwa na nafuu
.
Alihitaja Mikoa ambayo iko kwenye
mpango huu maalum ni Kigoma,Rukwa,Katavi,Mara ,Pwani na Tabora,hivyo
wanachama na wananchi kwa ujumla wajitokeze ili waweze kutumia fursa hii
muhimu na adimu kupata huduma za matibabu za madaktari bingwa.
CHANZO/MjengwaBlogs
No comments:
Post a Comment