IMANI za kishirikina zimezidi kukitisa Kijiji cha Isange na Kata ya
Isange baada ya matukio ya kupotea na kuawa kwa Watoto kutokea mara kwa
mara ambapo Marehemu hukutwa wakiwa na mapungufu ya viungo ikiwemo
Kichwa.
Katika tukio la hivi karibuni Mtoto mmoja aliyejulikana kwa Jina la
Lista Sebule (8) Mwanafunzi wa Darasa la Saba katika Shule ya Msingi
Mpombo iliyo katika Kata ya Isange Halmashauri ya Busokelo Wilaya ya
Rungwe Mkoani hapa alipotea katika mazingira ya kutatanisha na kukutwa
baada ya Siku 9 akiwa amekufa.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo akiwemo Mama mzazi wa
Marehemu Christina Sakalile alisema binti yake alipotea majira ya saa
tisa jioni Machi 31, Mwaka huu baada ya kutumwa kupeleka simu kibandani
ili kuchaji lakini hakurudi hadi Saa Kumi na Mbili jioni hali iliyozua
wasiwasi na kuanza kumtafuta bila mafanikio.
Alisema baada ya tukio hilo walitoa taarifa Kijijini ambapo
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Isange Daudi Nsyani ambaye baada ya kupewa
taarifa hizo pia aliwataarifu viongozi wa Kata akiwemo Diwani wa Kata ya
Isange Elias Mwasandele na Ofisa Mtendaji wa kata hiyo Brayson Nguro
ambaye aliitisha Mkutano wa wananchi.
Mtendaji huyo aliwaambia wananchi hao kushirikiana ili Mtoto
apatikane hali ambayoiliitikiwa na wananchi ambao walitaka Mtoto
apatikane aidha akiwa mzima ama Mfu ambapo juhudi za kumtafuta zilianza
na hatimaye kumpata Aprili 8, Mwaka huu akiwa amekufa huku akiwa hana
baadhi ya Viungo.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema Mwili wa Marehemu ulipatikana
ukiwa pembezoni ya Mto Nkalisi uliopo Kijijini hapo ukiwa umenyofolewa
baadhi ya viungo kama Kichwa na Miguu ambapo mguu mmoja ulipatikana
baada ya Mbwa kukutwa akiwa ameshika na kuudondosha baada ya kukutana na
watu hali iliyowalazimu watu hao kumfutilia Mbwa huyo aliyeongoza hadi
Mwili wa
Marehemu ulipokuwepo na kuwakuta Mbwa wengine wawili wakiwa
pembezoni.
Baada ya kupatikana kwa mwili huo Taarifa ilipelekwa Polisi ambao
walifika katika eneo la tukio na kuupima kisha kuwakabidhi ndugu kwa
ajili ya mazishi ambapo watu wawili walikamatwa kuhusika na tukio hilo
baada ya kupigiwa kura za siri na wananchi na kukutwa na kura nyingi
ambapo wengine wanne waliachiwa kutokana na kutokuwa na kura nyingi.
Kutokana na hali hiyo Ofisa Mtendaji wa kata hiyo alisema mfululizo
wa vitendo hivyo unatokana na kutokuwa na Vituo vya Polisi ambapo
Halmashauri ya Busokelo inakituo kimoja kilichopo katika Mji wa Lwangwa
mahali ambapo ni mbali sana kutokana na gharama kuwa kubwa.
Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo Elias Mwandele alisema wananchi
waache kutembea usiku ambapo aliongeza kuwa Vilabu vya Pombe vifungwa
saa mbili usiku huku akiwataka Wazazi kutowapeleka watoto kwenye
Shughuli za Machungo ambapo wameweka ulinzi wa Sungusungu ili kudhibiti
hali hiyo.
SAMAHANI KWA PICHA HII HATUJAIONYESHA VIZURI SABABU MWILI WA MTOTO
LISTA UMEHARIBIKA VIBAYA HIVYO TUMEONA SI VYEMA KUUONYESHA WOTE
MARA TU BAADA YA POLISI KUUTOA MWILI PORINI NA KUUCHUNGUZA
WALIWAKABIDHI WAZAZI ILI WAENDELEE NA TARATIBU ZA MAZISHI YA MTOTO
LISTA
MGUU WA MAREHEMU LISTA
MWANA USALAMA AKIWA AMEUSHIKA MGUU WA MTOTO LISTA MARA TU BAADA YA
KUUPATA MWILI WAKE PORINI NA KUKUTA HANA BAADHI YA VIUNGO VYAKE VYA
MWILI
UMATI MKUBWA ULIOHUDHURIA MAZISHI YA MTOTO LISTA
Source: Mbeya Yetu
No comments:
Post a Comment