DAVID Beckham akitimiza miaka 38, jana ameiongoza PSG kulazimisha sare ya 2-2 na Barcelona kwenye Uwanja wa Parc des Princes katika Robo Fainali ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Lakini matokeo hayo yanaiweka PSG katika
mlango wa kutokea, kwani sasa Barca wanapewa nafasi kubwa ya kusonga
mbele wakicheza mechi ya marudiano nyumbani.
Barcelona ilikuwa mbele kwa bao 1-0 hadi
mapumziko lililofungwa na mwanasoka bora wa dunia kutoka sayari
nyingine, Lionel Messi dakika ya 38.
Zlatan Ibrahimovic aliifunga timu yake
ya zamani kipindi cha pili (dakika ya 79) akiisawazishia PSG, lakini
Xavi akaifungia bao la pili Barca kwa penalti dakika ya 89.
Huwezi amini, dakika moja baadaye, PSG wakachomoa na safari hii alikuwa ni Matuidi aliyefunga bao hilo dakika ya 90.
Katika mchezo huo, kikosi cha PSG kilikuwa: Sirigu,
Jallet, Alex, Thiago Silva, Maxwell, Beckham/Verratti dk70, Matuidi,
Lucas Moura, Pastore/Gameiro dk76, Ibrahimovic na Lavezzi/Menez dk66.
Barcelona: Valdes,
Dani Alves, Pique, Mascherano/Bartra dk84, Jordi Alba, Xavi, Busquets,
Iniesta, Sanchez, Messi/Fabregas dk46, Villa/Tello dk81.
Utaipenda hii: Messi akitafuta mbinu za kumtoka Beckham
Safari: Messi sasa anamtoka Beckham
Amekula: Beckham amemkwatua Cesc Fabregas
Njano: Beckham akionyeshwa kadi ya njano na refa Wolfgang Stark
Amefunga tena: Lionel Messi akishangilia bao lake la kwanza jana
Bao la kusawazisha: Zlatan Ibrahimovic akishangilia bao lake la kusawazisha ambalo lililamikiwa kuwa la offside
Katika mchezo mwingine, Bayern Munich iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Juventus mjini Munich, shukrani kwao David Alaba na Thomas Muller wafungaji wa mabao hayo.
Hii kali: David Alaba aliifungia bao la kwanza Bayern Munich na hapa ndivyo alivyoshangilia
Chanzo/BinZubeiryBlogs.
No comments:
Post a Comment