MASHABIKI wa klabu za Manchester City na
West Ham wamepanga kumpa heshima kiungo Marc-Vivien Foe, aliyefariki
dunia miaka 10 iliyopita, wakati timu hizo zitakapokutana Aprili 27,
mwaka huu.
Kiungo huyo wa Cameroon alizimia kwenye
mechi ya Nusu Fainali ya Kombe la Mabara dhidi ya Colombia Juni 26,
mwaka 2003 kabla ya kufariki dunia muda mfupi baadaye akiwa na umei wa
miaka 28.
Foe, ambaye pia alizichezea Lens na Lyon
za Ufaransa, alifariki kutokana na matatizo ya moyo kama ambayo
yalitaka kuuchukua uhai wa kiungo wa Bolton, Fabrice Muamba aliyezimia
uwanjani mwaka jana.
Shukrani Muamba aliepuka kifo, lakini baadaye akaamua kustaafu soka.
Kioo: Marc-Vivien Foe aliichezea West Ham (kushoto) kabla ya kupelekwa kwa mkopo Manchester City (kulia)
Kazini: Marc-Vivien Foe (kushoto) akipambana na Juan Sebastian Veron wa Man United akiwa Manchester
Upendo wa hali ya juu: Foe akimkumbatia mchezaji mpya wakati Paolo Di Canio West Ham Januari 1999
West Ham ilimsajili Foe kwa Pauni
Milioni 4.2 mwaka 1999 kabla hajarejea Ufaransa kujiunga na Lyon mwaka
2000. Baadaye alijiunga na City kwa mkopo mwaka 2002 na akaifungia mabao
tisa. Alikuwa mchezaji wa mwisho kufunga kwenye Uwanja wa City wa
zamani, Maine Road.
Tangu kifo chake, klabu hiyo iliacha kuitumia jezi namba 23 ambayo alikuwa akiivaa Foe.
Kipenzi cha mashabiki: Foe (kulia) alikuwa kipenzi cha mashabiki wote West Ham (juu) na City nchini England
Goalscoring touch: Foe rounds Aston Villa keeper Peter Enckelman to help City to a 3-1 win at Maine Road
Janga: Foe alifariki katika mchezo kati ya Cameroon na Colombia
Masikini: Mchezaji wa Colombia, Jairo Patino akimuwahi Foe baada ya kuanguka uwanjani.
CHANZO/BinZubeiryBlogs.
No comments:
Post a Comment