Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akikata utepe kuifungua Nyumba
ya Walimu Skuli ya Kusini Makunduchi, iliyojengwa na Jumuiya ya ya
Maendeleo ya Makunduchi Mzuri kaja,kwa ushirikiano na Jumuiya ya Bus 4
Afrika,yenye Makao Makuu yake nchini Sweden
Mwakilishi wa Jumuiya ya Bus 4 Afrika
yenye Makao Makuu yake Nchini Sweden Bibi Hannah Mc Carrick,akitoa salam
wakati wa Sherehe ya Ufunguzi wa Nyumba ya Walimu Skuli ya Kusini
Makunduchi,iliyojengwa na Jumuiya hiyo na Ushirikiano wa Jumuiya ya
Maendeleo ya Makunduchi Mzuri kaja, iliyofunguliwa na Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Ali Juma Shamuhuna akimkaribisha Dkt. Shain kuzungumza na wananchi kwenye uzinduzi huo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Wananchi na
Wanajumuiya ya Maendeleo ya Makunduchi Mzuri kaja,Wilaya ya Kusini
Unguja, wakati wa Sherehe ya Ufunguzi wa Nyumba ya Walimu Skuli ya
Kusini Makunduchi, iliyojengwa na Jumuiya ya ya Maendeleo ya Makunduchi
Mzuri kaja,kwa ushirikiano na Jumuiya ya Bus 4 Afrika ya Sweden.
Picha
na Ramadhan Othman, IKULU-Zanzibar.
CHANZO/MjengwaBlogs.
No comments:
Post a Comment