Rais
mpya wa awamu ya nne nchini Kenya,Mh Uhuru Kenyatta akiwapungia maelfu
ya watu waliofika kushuhudia kuapishwa kwake, mapema leo kwenye sherehe
iliyofanyika kwenye uwanja wa Kasarani,jijini Nairobi Sherehe hizo
zimehudhuriwa na Marais kutoka nchi mbalimbali akiwemo Rais wa Jamuhuri
ya Muungano wa Tanzania,Mh Jakaya Mrisho Kikwete,Mabalozi mbalimbali na
watu mbalimbali.Picha zote kwa hisani ya Mike Kariuki wa Capital FM.
Rais
mpya wa awamu ya nne nchini Kenya,Mh Uhuru Kenyatta akisoma hotuba yake
mbele ya maelfu ya watu waliofika kushuhudia kuapishwa kwake, mapema
leo kwenye sherehe iliyofanyika ndani ya uwanja wa Kasarani,Sherehe hizo
zimehudhuriwa na Marais wa nchi mbalimbali ambapo Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania,Mh Jakaya Mrisho Kikwete amehudhuria.
Rais mpya wa awamu ya nne nchini Kenya,Mh Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta akisalimiana na Makamu wake William Ruto.
Rais
Uhuru Kenyatta akila kiapo cha Urais,kuwa rais wa awamu ya nne nchini
Kenya,kwenye sherehe zilizofana kwa kiasi kikubwa ndani ya uwanja wa
kasalani.
Rais
wa Uganda,Mh Yoweri Kaguta Museven akisoma hotuba yake fupi wakati wa
kuapishwa kwa Rais wa awamu ya nne nchini Kenya,kwenye sherehe
zilizofanyika ndani ya uwanja wa Kasalani,jijini Nairobi.
No comments:
Post a Comment