MWENYEKITI
wa Chama cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba, amesema theruthi
tatu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wanakabiliwa na umasikini wa
kutisha kutokana wakazi wake kuishi kwa sh 640 kwa siku.
Akizungumza na
wandishi wa habarijijini jana, Lipumba alisema
Kongamano la kujadili maendeleo ya mkoa huo,limeandaliwa na chama
chake,Taasisi ya Demokrasia ya nchini Denmark huku washiriki 130 kutoka
taasisi za serikali, viongozi wa dini na mashirika.
Lipumba
alisema chimbuko la umasikini huo ulichangiwa na ongezeko la watu huku
wengi wao wakikabiliwa na ukosefu wa ajira za kuelewka.
Alisema
jiji hilo lenye idadi ya wakazi wapatao milioni 4.5, kati ya hao ni
milioni 1.3 wenye ajira, wengine ajira zao ni zile za kubahatisha.
“Haingii
akilini kwa maisha ya jiji la Dar es Salaam mtu aweze kuishi kwa sh 640
hii si kweli, wote tunajua maisha ya jiji hili yalivyo”alisema.
Katika kupunguza tatizo la ajira, Lipumba alisema mikakati ya makusudi ya kuanzisha viwanda ambavyo vitachechemua uchumi.
Alivitaja
baadhi ya viwanda hivyo ni vya ngozi, mavazi, umeme, viatu na vingine
ambapo alitahadharisha kuwa kusiwe na urasimu kwa watu watakaojitokeza
kwa ajili ya kutaka kuanzisha viwanda hivyo.
Aidha,
sekta ya elimu bado inakabiliwa na changamoto lukuki ambazo zinahitaji
mjadala mpana katika ambao utasaidia kuupatia ufumbuzi wa kudumu.
Alisema
bila ya kuwa na elimu bora ambayo itazalisha wataalamu mbambali
wakiwemo wale wa sayansi, nchi hii haiwezi kusonga mbele kimaendeleo,
ambayo ni kiu ya muda mrefu kwa wananchi.
“Na
hii elimu yetu bado inakabiliwa na matatizo kutokana watoto wetu
kufundishwa lugha ya Kiswahili na wanapofika sekondari lugha inayotumika
ni kingereza hali inayowafanya wafeli mitihani yao”alisema.
Ukiachilia
mbali wanafunzi hao kushindwa matumizi ya kingereza bado wapo ambao
wanamaliza elimu ya msingi hawajui kusoma vitabu vya Kiswahili.
Baadhi
ya washiriki kwa nyakati tofauti walisema ukusanyaji wa makato bado
katika Halmashauri hauridhishi, wakati mwingine yanayokusanywa ni
asilimia 40 lakini mipango yake yanazidi ya kawaida kwa asilimia 70.
Mratibu
wa Kongamano na Taasisi ya vyama na Demokrasia (DIPD), Anemon
Birkebaek, alisema atatumia uzoefu wake kwa kuwaunganisha vijana wa
Denmark na wapa ili waweze kubadilishana uzoefu katika kujiletea
maendeleo.
CHANZO/MjengwaBlogs.
No comments:
Post a Comment