KLABU ya Bayern Munich wameanza vyema
kampeni ya kuelekea kucheza fainali ya tatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya
ndani ya miaka minne, baada ya kuikung'uta Barcelona mabao 4-0 usiku
huu kwenye Uwanja wa Allianz Arena katika Nusu Fainali ya kwanza.
Mabao mawili kutoka kwa Thomas Muller na
moja kwa kila mmoja, Mario Gomez na Arjen Robben yamempa faraja kocha
Jupp Heynckes ambaye sasa sijui itokee miujiza gani Jumatano ijayo
Uwanja Nou Camp kwenye mchezo wa marudiano akose tiketi ya kwenda
Wembley.
Kikosi cha Bayern Munich kilichofanya
mauaji hayo kilikuwa: Neuer, Lahm, Boateng, Dante, Alaba, Javi Martinez,
Schweinsteiger, Robben, Muller/Pizarro dk83, Ribery/Shaqiri dk88 na
Gomez/Gustavo dk71.
Barcelona: Valdes, Dani Alves, Pique, Bartra, Jordi Alba, Xavi, Busquets, Iniesta, Sanchez, Messi na Pedro/Villa dk83.
Mbele kwa mbele: Thomas Mueller akishangilia baada ya kuifungia Bayern bao la kwanza
Mguu mmoja fainali: Nyota wa Bayern
Munich, Mario Gomez na mchezaji mwenzake, Javi Martinez wakishangilia
baada ya kupata bao la pili
La tatu kiulainiiii: Arjen Robben akishangilia baada ya kufunga bao la tatu dhidi ya Barca
kumbuka jina: Robben akishangilia mbele ya mashabiki baada ya kufunga bao lake
Wapoleee: Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi akionekana aliyekata tamaa
Hakuna kurudi nyuma? Messi na Barcelona wanakabiliwa na mchezo mgumu wa marudiano.
CHANZO/BinZubeiryBlogs
No comments:
Post a Comment