Kamishna
wa Idara ya Sera ya manunuzi ya umma kutoka wizara ya Fedha Dk.
Frederick Mwakibinga (kulia) akiongea jambo na Clemence Tesha ambaye ni
mjumbe wa kamati ya sera ya manunuzi wakati wa kongamano la kujadili
rasimu ya sera ya manunuzi ya umma lililofanyika hivi karibuni jijini
Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja lilihudhuliwa na wajumbe
mbalimbali kutoka ofisi za Serikali na Taasisi binafsi.PICHA NA ANNA NKINDA
Emmanuel
Maliganya ambaye ni Afisa Ugavi kutoka Benki Kuu ya Tanzania
akichangia mada kuhusu utendaji kazi wa maafisa ugavi wakati wa
kongamano la kujadili rasimu ya sera ya manunuzi ya umma lililofanyoka
hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja
liliandaliwa na Idara ya Sera ya manunuzi ya umma kuhudhuliwa na wajumbe
mbalimbali kutoka ofisi za Serikali na Taasisi binafsi. Juma
Fimbo kutoka Umoja wa wataalamu wa Manunuzi na Ugavi Tanzania
akielezea jinsi maafisa ugavi wanavyotakiwa kufanya kazi zao kwa kutumia
taaluma ya uchumi wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya sera ya
manunuzi ya umma lililofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Kongamano hilo la siku moja liliandaliwa na Idara ya Sera ya manunuzi ya
umma na kuhudhuliwa na wajumbe mbalimbali kutoka ofisi za Serikali na
Taasisi binafsi. Mkurugenzi
wa Ugavi kutoka Akaunti ya Changamoto za Milinia (Millenium Challange
Account) Marieth Ngaida akichangia mada wakati wa kongamano la kujadili
rasimu ya sera ya manunuzi ya umma lililofanyika hivi karibuni jijini
Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja liliandaliwa na Idara ya Sera
ya manunuzi ya umma. Prof.
Gaspar Munishi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Sayansi ya
Siasa na Utawala akielezea kuhusu umuhimu wa kuboresha rasimu ya Sera
ya manunuzi wakati wa kongamano la kujadili rasimu hiyo lililofanyika
hivi karibuni katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa JB jijini Dar es
Salaam. Kongamano hilo la siku moja liliandaliwa na Idara ya Sera ya
manunuzi ya umma. Kulia ni Dk. Godfrey Sansa kutoka Chuo hicho. Kamishna
wa Idara ya Sera ya manunuzi ya umma kutoka Wizara ya Fedha Dk.
Frederick Mwakibinga (kushoto) akisalimiana na Prof. Gaspar Munishi
kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Sayansi ya Siasa na
Utawala wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya Sera ya manunuzi ya
Umma lililofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano
wa JB jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja lilihudhuliwa
na wajumbe mbalimbali kutoka ofisi za Serikali na Taasisi binafsi. Baadhi
ya wajumbe kutoka ofisi za Serikali na Taasisi binafsi wakimsikiliza
Prof. Gaspar Munishi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya
Sayansi ya Siasa na Utawala (hayupo pichani) wakati wa kongamano la
kujadili rasimu ya Sera ya manunuzi ya Umma lililofanyika hivi karibuni
jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja liliandaliwa na Idara
ya Sera ya manunuzi ya umma. Khamisi
Tikka kutoka Mamlaka ya Rufaa za zabuni akichangia mada wakati wa
kongamano la kujadili rasimu ya Sera ya manunuzi ya Umma lililofanyika
hivi karibuni katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa JB jijini Dar es
Salaam. Kongamano hilo la siku moja liliandaliwa na Idara ya Sera ya
manunuzi ya umma na kuhudhuliwa na wajumbe mbalimbali kutoka ofisi za
Serikali na Taasisi binafsi.
CHANZO/MjengwaBlogs
No comments:
Post a Comment