MABAO
manne ya Robert Lewandowski usiku huu yameipa Borussia Dortmund ushindi
wa 4-1 dhidi ya Real Madrid katika Nusu Fainali ya kwanza ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya nchini Ujerumani.
Mabao
hayo ya mshambuliaji huyo wa Poland yanawafanya Dortmund watengeneze
mazingira ya fainali ya klabu za Ujerumani tupu itakayopigwa Uwanja wa
Wembley mwezi ujao, kufuatia jana Bayern Munich kuichapa 4-0 Barcelona
nchini Ujerumani pia.
Lewandowski alifunga bao la kwanza dakika ya nane, kabla ya Cristiano Ronaldo kuisawazishia Real dakika ya 43.
Lakini
mshambuliaji huyo akarudi na makali zaidi kipindi cha pili na kufunga
mabao matatu zaidi dakika za 50, 55 na 67 kwa penalti.
Kocha
wa Real, Mreno Jose Mourinho aliyekuwa 'hoi' uwanjani baada ya kipigo
leo, sasa anatakiwa kutengeneza mipango ya kushinda 3-0 katika mchezo wa
marudiano wiki ijayo, ili kuwapiku Dortmund.
Kikosi
cha Borussia Dortmund kilikuwa: Weidenfeller, Piszczek/Grosskreutz
dk83, Subotic, Hummels, Schmelzer, Bender, Gundogan/Schieber dk90,
Blaszczykowski/Kehl dk82, Gotze, Reus na Lewandowski.
Real
Madrid: Diego Lopez, Sergio Ramos, Varane, Pepe, Fabio Coentrao,
Khedira, Alonso/Kaka dk80, Ozil, Modric/Di Maria dk68, Ronaldo na
Higuain/Benzema dk68.
Moto: Robert Lewandowski amefunga mabao yote manne ya Dortmund dhidi ya Real Madrid leo
La kwanza: Lewandowski akiifungia Dortmund bao la kwanza
La kusawazisha: Cristiano Ronaldo aliisawazishia Real Madrid na kipindi cha kwanza kiliisha 1-1
La pili: Lewandowski akifunga la pili
No comments:
Post a Comment